Mwanamuziki wa Bongo Flava   Abedinego Damian, ‘Belle 9′ atoa ya moyoni na kusema kuwa Uzungu mwingi kwenye nyimbo zake sio sababu ya yeye kufeli katika Muziki.

Belle 9 anayetamba na kibao chake cha  Take Away ambaye anatamba na Ngoma ya Take alisema kwanza hajafeli kimuziki, nyimbo anazotoa zinakubalika sana na muziki ni hisia hata uimbe lugha gani kama unakipaji watu wanaelewa kile unachoimba.

Ameenda mbali zaidi na kusema “Lugha kwenye muziki inanafasi ndogo sana kuliko kipaji cha mtu na uwezo wake. Kuna nyimbo za Kikongo hapa zinasikilizwa sana na watu utasema wanaelewa Kikongo au Kilatino. Muziki unazungumza na mtu yeyote kwa lugha yoyote ile kwa hiyo madai hayo hayana mashiko, mashabiki zangu waendelee kunisapoti na kufurahia muziki mzuri kutoka kwangu,” alisema Belle 9.