Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ben Pol amewataka wasanii wenzake kutokata tamaa kwa kilichowatokea huko nchini Uingereza, kwa kupata muitikio mdogo wa watu katika shoo ambayo walikuwa wameandaliwa waifanye.

Ben Pol ameeleza hayo baada ya kuenea uvumi kwenye mitandao ya kijamii ikiwahusisha wakina Aslay, Ray C, Temba pamoja na Rosa Ree kuwa shoo yao ili buma kutokana na muamko wa watu waliojitokeza ukumbini.

Aidha, Ben Pol amedai laiti suala hilo lingekuwa limemtokea yeye asingeweza kuacha kuimba hata kama angekuwa amejitokeza mtu mmoja pekee yake.

“Muziki ni kazi yangu hivyo hata kama angetokea mtu mmoja kwenye shoo, mimi ningeimba kama vile ambavyo ningewaimbia watu 100, kwasababu hatua ya mtu mmoja kulipa fedha yake huenda akitoka hapo ukumbini atapeleka sifa nzuri kwa mashabiki wengine ambao hawakujitokeza”,¬†amesema Ben Pol.

Katika miaka ya hivi karibuni, wasanii wengi wamekuwa wakipata matatizo mengi wanapokuwa wameandaliwa shoo za nje ya nchi, ikiwemo na hilo la mashabiki kususia kuingia ukumbini bila ya kuwepo sababu za msingi zinazo kuwa zimebainishwa kutoka kwa promota.