Rapper Chemical amesema kuna kipindi alikuwa akipata wakati mgumu sana kuhusu mavazi yake, kuna watu walikuwa wakimshauri avae nguo za kike na wengine wakimwambia avae za kiume, ila yeye alifanya maamuzi magumu ya kuwasikiliza mashabiki wake ndio maana kwa sasa anachanganya mavazi yote.
Fid Q ameponda Marap wa Kike wanaovaa nguo za kiume wakiona kuwa ndo fashion wakati imepitwa na wakati, Amemsifia Rapa Rosa Ree kwa kudai kuwa anavaa nguo za kike kama mwanamke na bado anafanya vizuri katika game ya Rapu