stori iliyotawala Kwenye mitandao ya kijamii ni Tetesi za Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Rose Alphonce maarufu kama Muna Love.

Global Publishers waliripoti kuwa ndugu wa karibu wa Muna ndio wamemnyooshea kidole kwa kitendo chake cha kumtelekeza mtoto wake Nyumbani kwao Moshi.

Baada ya taarifa hizo kuzagaa Mtandaoni Muna alikana kabisa na kusisitiza wanaosambaza taarifa hizo wana nia moja tu ya kumchafua ili aonekane mbaya.

Siku ya leo Muna Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa Mtu ambaye amesambaza taarifa hizo yuko mikononi mwa polisi na ambaye amemtuma ni mama yake mzazi na dada yake: