Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro ameonya wale wote watakaojaribu kufanya fujo wakati wa Chaguzi ndogo katika Majimbo ya Ukonga na Monduli kuwa watachukuliwa hatua kali kwa kuwa Jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafanyika kwa amani na utulivu.

IGP Sirro ameyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam baada ya  kuzungumza na Askari watakaosimamia zoezi hilo  leo katika Jimbo la Ukonga ambapo amesisitiza kila mmoja kuwa makini katika kusimamia zoezi hilo.

Aidha IGP Sirro amewataka Wananchi kutambua wajibu na mara wamalizapo kupiga kura kurudi nyumbani ili kusubiria matokeo.