Kampeni za udiwani kata ya Vingunguti leo zimefikia mwisho ambapo katibu wa NEC  itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole amewataka wananchi wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi kesho jumapili kumpigia kura Mgombea wa CCM, Omary Said Kumbilamoto.

Kampeni za  udiwani kata ya Vingunguti Zimefungwa leo katika uwanja wa Msikatetamaa, ambapo Polepole alikuwa mgeni rasmi na kueleza kuwa chama cha Mapinduzi chini ya mwenyekiti wake Dr John Pombe Magufuli kimefanikiwa  mambo mengi ya maendeleo  ambapo hata wapinzani wamekosa hoja za msingi.

“Watu wenye akili zao vijana na kama Kumbilamoto Mtatiro na akinamama wameona Mazuri ya CCM na kuamua kumuunga mkono Rais, nami na waaomba  kesho Septemba 16 wakazi wa Vingunguti mpigieni kura Omary Said Kumbilamoto mapema tu tuwe tumeshinda jina lake kwenye karatasi litakuwa nambambili”amesema

Viongozi wengine waliomwombea kura Kumbilamoto ni pamoja na mbunge wa Ilala Musa Azan Zungu , Bonna Kaluwa, wa Segerea, Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Dar es salaam Frank Kamugisha na Julius Mtatiro aliyejiunga na CCM akitokea CUF  na Wenyeviti saba wa Mitaa ya kata hiyo.

Katika hatua nyingine Diwani wa kata ya Buguruni kwa mnyamani Shukuru Dege leo amejivua uanchama wa Chama cha wananchi CUF na kujiunga na CCM, ambapo amesema ameamua kujiunga na CCM kwa kuwa CUF imepoteza mwelekeo na pia ameamua kuunga mkono serikali ya awamu ya tano.

Pamoja na hayo Mgombea wa kata hiyo Omary Said Kumbilamoto amesema amefurahishwa na wananchi wa kata hiyo kwa kumuunga mkono na kuwaomba tena kesho kumpigia kura kwa wingi iliaendeleekuwatumikia  akiwa CCM na kuwaletea maendeleo.