Msanii wa Filamu Bongo, Jackline Wolper amesema ndoto yake kubwa ni kumvisha msanii wa Marekani, Rihanna.

Wolper ambaye ni Mbunifu wa Mavazi pia ametaja wasanii wengine kuwa ni Cardi B na Nicki Minaj.

“Mimi hapa Jackline Wolper siku isiyo na jina nitawavalisha Rihanna, Cardi B au Nicki Minaj maana wale ndio wana swag zangu.

“Nitaanza na Rihanna kwa sababu ndio mchizi wangu, mambo yake ndio yangu, yaani mimi ndio Rihanna wa Bongo. She don’t care anafanya maisha yake, anavaa kile anachojisikia akiona yeye amependeza basi amependeza, ndio mimi,” Wolper ameiambia Wasafi TV.

Jackiline Wolper ni Mbunifu wa Mavazi kupitia duka lake linalokwenda kwa jina la House of Stylish