Baada ya klabu ya Simba ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara kutoka sare na Ndanda FC, msemaji wa timu hiyo Haji Manara ametoa neno kwa mashabiki.

Kupitia mtandao wa Instagram, Manara ameandika ujumbe ambao unaonekana ni kuwapooza hasira mashabiki wa timu hiyo ambao walikuwa na matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo kutokana na maandalizi mazuri ya timu yao.
Kupitia mtandao huo Manara ameandika, “This is a marathon not a sprint. Much respect to Ndanda FC for playing with the champions and Lions of the country!!! And the equal result as well ofcourse!! You have fought a good fight.”
Kutokana na matokeo hayo Simba inabakia kwenye nafasi yake ya tatu ikiwa na alama saba wakati Ndanda imepanda mpaka nafasi ya 12 wakiwa na alama nne.