Baba Mzazi wa Pancho Latino Asema  Atazikwa Jumamosi Gairo Mkoani Morogoro

Baba Mzazi wa muandaaji wa muziki nchini Tanzania, Marehemu Pancho Latino amesema kuwa mtoto wake atazikwa kijijini kwao Msingisi Wilani Gairo mkoani Morogoro.
Mchungaji Simon Magawa amesema kuwa kwa mara ya kwanza alizipata taarifa za kifo cha mtoto wake kupitia mitandao ya kijamii na baadae akampigia kaka wa marehemu ambaye alikuwa anaishi naye hapa Dar es salaam.

Kuhusu ratiba ya mazishi Mchungaji Magawa amesema kuwa mtoto wake atazikwa kijijini hapo siku ya Jumamosi endapo ratiba itaenda kama ilivyopangwa.