Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu Irene Pancras Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa uongozi wake mpya ndio unahakikisha anaishi maisha mazuri.

Global Publishers wanaripoti kuwa Uwoya amekuwa akila bata kwenye viwanja vya gharama kubwa ikiwemo mahoteli makubwa huko Dubai, Zanzibar na mikoani hivyo kuibua maswali kwa mashabiki wake kuwa ni mapato ya filamu tu au?

Mbali na matanuzi na shopping za nguvu, Uwoya amekuwa akibadili magari makali huku akiendelea na ujenzi wa klabu yake ya gharama kubwa ya Last Minute iliyopo Sinza- Mori jijini Dar.

Kwenye mahojiano man gazeti la Ijumaa Uwoya aliulizwa kuhusu matanuzi hayo na endapo kuna mtu mwingine zaidi ya Mumewe Dogo Janja anasimamia ambapo  alifunguka:

Hakuna mtu, unajua sipendi kuweka mambo yangu hadharani. Haya ndiyo maisha yangu, ni kawaida.

Kuhusu nguo mpya kila siku Ni mimi tu nimeamua kupendeza. Kama ni kubadili nguo mimi nguo ninazo nyingi sana, sema zamani nilikuwa navaa, lakini sipigi picha. Nadhani hii ishu ya kuvaa na kuposti mtandaoni ndiyo inafanya watu waone ni nguo mpya”.

Lakini pia Uwoya alitoa siri ya kuwa na Management kwa sasa ambayo inahakikisha anajijengea image ambayo anayo kwa sasa kama Msanii:

Kuna siri watu wengi hawaijui. Kwa sasa mambo yote yanasimamiwa na menejimenti yangu. Menejimenti ndiyo inanifanyia kila kitu ambacho watu wanaona ni jeuri ya fedha”.

Kutokana na maisha anayoishi hivi sasa Uwoya kuna tetesi zilikuwa zinadai kuna Kigogo mmoja mwenye pesa ndefu ndio anasimamia lifestyle ya Uwoya kutokana na ukweli Mumewe Dogo Janja hawezi kumfanyia mambo makubwa.