Mama Wema Adaiwa Kumfanyia Vurugu Bwana Wa Wema

Mama mzazi wa staa wa Bongo movie Wema Sepetu, Miriam Sepetu maarufu kama Mama Wema amedaiwa kumfanyia bonge la varangati mwanaume ambaye alikuwa  mpenzi wa Wema, R.a.h.u.r.

Global Publishers wanaripoti kuwa Mama Wema ambaye hakuwa akifurahishwa sana na uhusiano wa bintiye na ‘mkwewe’ huyo, aliibuka nyumbani hapo kwa mwanaye na kumtolea uvivu baada ya kuona jamaa si mtu wa maana.

Inaripotiwa kuwa siku ya tukio Mama Wema alienda nyumbani kwa Wema maeneo ya Salasala lakini alipofika hakumkuta mwanaye zaidi ya yule mwanaume na inadaiwa baada ya muda umeme uliisha na Mama Wema alipoona kijana yule hana mpango wa kununua alimtimua na kumfanyia bonge la varangati.

Baada ya sakata hilo gazeti hilo lilimsaka Mama Wema ili kupata ukweli wake ambapo alifunguka haya kwa upande wake:

Hakuna mwanaume yeyote ambaye Wema amenitambulisha hivyo ndiyo maana nilimtimua. Naona na kuyasikia haya mambo kwenu waandishi, lakini hakuna mtu ambaye mimi namfahamu yupo na mwanangu”.

Lakini pia mwanaume ambaye alikuwa katikati ya sakata hilo alisakwa na kufunguka ambapo amekana kabisa taarifa hizo:

Si kweli kwamba mimi nimegombana na huyo mama kwa sababu eti ya luku, mimi nashindwa kununua luku ukiniangalia? Huyo mama hakutaka niwe karibu na mwanaye kwa madai sijui hayuko vizuri anaumwa”.

GPL pia wameripoti kuwa Wema na mwanaume huyo kwa sasa wameachana na Wema tayari yupo na jamaa mwingine ambaye hataki kabisa kumuweka hadharani.