Mwimbaji wa nyimbo za Injili Bongo, Emmanuel Mbasha amepagawa baada ya kupewa majibu ya Ukimwi ambayo alienda kupima.

Chanzo ambacho ni mtu wa karibu wa Mbasha kilieleza kwamba mwanamuziki huyo alikwenda kupima Virusi Vya Ukimwi (VVU) na alipopatiwa majibu alijikuta akirukaruka kama yuko jukwaani akiimba nyimbo zake.

“Mbasha, baada ya kupata majibu kwamba ni mzima, hanamaambukizi ya Virusi Vya Ukimwi alipagawa yaani kama mtu ambaye alikuwa aamini, hapo ndiyo utajua kila mtu duniani anaogopa Ukimwi iwe mtumishi wa Mungu au mtu wa kawaida,” kilieleza chanzo hicho.Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Mbasha ambaye alikiri kupima ngoma na kujikuta akipagawa kwa furaha kutokana na kukutwa hana maambukizi.

“Nilijikuta ninapagawa kwa sababu ya ile furaha ya kukutwa mzima wa afya na siyo kwamba nilikuwa sijiamini, unajua ukimwi hauambukizwi kwa ngono tu unaweza kupata kwa njia mbalimbali kwa hiyo hapa nina furaha ya ajabu,” alisema Mbasha.