IKIWA hitimisho la bethidei yake aliyoifanya kwa wiki nzima lilikuwa Jumapili iliyopita ambapo alisherehekea ndani ya boti, uzungu wa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na dada’ke, Esma Khan umezua gumzo, Risasi Mchanganyiko linakupa mkanda kamili.

Katika sherehe hiyo iliyofanyika ndani ya boti katika Bahari ya Hindi, Dar, ilihudhuriwa na watu wa karibu yaani wanafamilia na marafiki wachache wa Diamond.

Ndani ya boti waalikwa walijiachia vya kutosha huku kila mmoja akionekana kupendeza kwani wengi walikuwa wamevaa nguo nyeupe. Pamoja na kupendeza huko miguno na gumzo kubwa lilikuwa ni kwa Diamond na Esma ambao walionekana wakijiachia kwa pozi tata tofautitofauti.

Diamond na dada yake walipiga picha wakiwa kwenye pozi huku wakiwa wameshikilia glasi za vinywaji ambapo Mbongo-Fleva huyo alikuwa kifua wazi huku Esma akiwa mapaja wazi. Waliohudhuria katika sherehe hiyo na wale walioiona katika mitandao ya kijamii walipigwa na butwaa huku wakieleza kwani zaidi huwa linakaliwa na watu ambao ni wapenzi.

“Yaani huu uzungu wa Diamond na dada yake huu mh! Sijauelewa kabisa maana watu ambao ni ndugu mmezaliwa tumbo moja kujiachia vile kama wapenzi siyo sawa hata kama wako ufukweni, kiukweli wanatakiwa kujirekebisha kwani hayo siyo maadili ya Kitanzania.

“Wasanii wetu wanaathiriwa sana na kuiga mambo ya kizungu ambayo baadaye yanaweza kuwaletea madhara makubwa kwani wanaweza kujikuta hata wanajiingiza kwenye hatari wakiendekeza uzungu,” alisema mmoja wa waalikwa walioshuhudia ukaribu wa ndugu hao.

Diamond alikuwa akisherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa Oktoba 2, mwaka huu ambapo iliendelea mpaka Oktoba 7, mwaka huu ambayo ilikuwa ndiyo hitimisho. kuwa siyo maadili kwa kaka na dada kukaa katika pozi la aina hiyo.