Rais Magufuli Amtuma Salam za Rambirambi Rais Kenyatta Kufuatia Ajali Iliyoua Watu Zaidi ya 50

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ametuma salam za kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kufuatia ajali iliyoua watu zaidi ya 50 katika eneo la Kericho nchini humo.

Kupitia ukurasa wa Twitter wa Rais Magufuli ameandika “Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya basi iliyotokea Kericho nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50. Nakupa pole Rais Uhuru Kenyatta, familia za marehemu na Wakenya wote. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema na majeruhi wapone haraka.”