Waziri TAMISEMI, Suleiman Jaffo amemuagiza Ronald Lwakatare kujieleza mara moja ni kwanini huduma za usafiri zinasuasua na kusababisha adha kwa wakazi wa Mkoa wa Dar

Pia amemtaka Naibu Waziri TAMISEMI, Joseph Kakunda kukutana kesho na Menejiment ya DART pamoja na UDART kujua nini kiini cha matatizo yanayoukumba usafiri huo

Aidha, amemtaka Katibu Mkuu TAMISEMI, Mhandisi Musa Iyombe kuchunguza kama kuna Watendaji wa DART wanahujumu mradi huo na wachukuliwe hatua za haraka ikiwemo kusimamishwa kazi.