The Art Of Self Destructions kama Mwanachana wa CCM na Raia wa Tanzania nimeshitushwa sana na kauli za hivi karibuni za Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kama nilivyowasoma kwenye post iliyopita Katibu Mkuu wa CCM ana haki za kikatiba kusema ukweli so NA MIMI NAOMBA MNIPE RUHUSA NITUMIE HAKI ZANGU ZA KIKATIBA kutoa maoni yangu kufuatia hizi kauli..(1)… CCM haiwahitaji Wasanii Majukwaaani tena ..(2). .Serikali ya Awamu ya Nne haikuwa na uhalali wa kisiasa …(3)…Wananchi wanaona hizi Chaguzi ni Kituko na Maigizo ….kwa uzoefu wangu wa Siasa za Taifa these are very serious and sensitive statements kutolewa na Secretary General wa Chama Kinachotawala na the Worst one ni kauli inayosema Awamu ya Nne haikuwa na Uhalali wa kisiasa kama ninamuelewa vizuri ni kwamba Serikali ya sasa inatokana na Serikali iliyopita sasa kama kauli yake inasimama kama ilivyo Serikali ya sasa inapata wapi uhalali huo kama Serikali iliyowaachia kijiti haikuwa na Uhalali? ….I mean hivi ni kweli Katibu Mkuu wa CCM anatuambia kwamba kitu kisicho halali kinaweza kuzaa matunda halali? …Anasema CCM haiwahitaji tena Wasanii wakati anajua fika kazi kubwa iliyofanywa na Wasanii kwenye Kampeni zilizopita ambazo ziliishia kukipa CCM madaraka mpaka na yeye kupata madaraka hayo leo anaukata mti alioukalia bila kufikiri mara mbili wala kuwauliza waliomtangulia? Kuna nini huko CCM? …hizi zilitakiwa kuwa kauli za Kikao cha CCM aidha NEC au Kamati Kuu lakini sio Kiongozi mmoja wa Juu kama yeye peke yake on a serious note something is not right …nilidhani Media huwa zina mnukuu kimakosa lakini kadri siku zinavyokwenda kauli zake zinazidi kuwa za utata zaidi kuliko za kwanza …upinzani ambao majuzi walimshambulia sana alipowajia juu waandishi wa habari kwamba hataki maswali ya kupima integrity yake, leo wanamshangilia kwamba ni msema ukweli ….UNAFIKI AT BEST….hahahahaha….Guys The best American President ever Ronald Reagan originally alikua Democratic Party lakini akafika mahali Mwaka 1962 baada ya kuona hakubaliani na sera za Chama chake aliamua kujitoa na kujiunga na Upinzani …KWA HIZI KAULI HUENDA SG WETU ANAHITAJI KUFANYA MAAMUZI MAGUMU NOW!..PLEASE!