Msanii mkongwe wa muzikik wa dansi nchini, Ali Choki baada ya siku chache zilizopita kuwa hoi akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari, mapafu na presha kwa sasa anafurahi baada ya hali ya afya yake kuzidi kuimarika.

Akizungumza na Risasi Vibes, Choki alisema kwa sasa anaendelea vizuri tofauti na ilivyokuwa mwanzo hivyo Mungu akipenda mwishoni mwa mwezi huu ataendelea na kazi ya muziki katika bendi anayoitumikia kwa sasa ya Super Kamanyola jijini Mwanza.

“Nina furaha kwani kwa sasa naendelea vizuri, hali yangu inaimarika kila siku, Mungu akipenda mwishoni mwa mwezi huu nitapanda jukwaani kama kawaida kwa ajili ya kuwapagawisha mashabiki wangu,” alisema Choki.

SHARE
Previous article
Next articleMKE WA ROMA AFUNGUKA MUMEWE AKILEWA