Baada ya Kutemana na Esma Petit Man Amishia Mapenzi kwa Mtoto wa Gardner Mwenyewe Afunguka A-Z

MENEJA wa wasanii mbalimbali Bongo, Hemed Manungwa ‘Petit Man’ amefungukia madai ya kutoka kimapenzi na mtoto wa mtangazaji wa Redio Clouds FM, Gardner Habash, Careen kwa kusema madai hayo hayana ukweli wowote.
Petit alisema anashangaa kuona watu wanasambaza umbea mitandaoni kuwa anatembea na Careen, kitu ambacho si cha kweli na binti huyo anamchukulia kama mdogo wake na ni marafiki pia.
“Watu wanasema sana juu yangu na Careen lakini hawaelewi yule ni kama mshikaji lakini kingine ni kama mdogo wangu wa karibu sana hivyo siwezi kuwaziba midomo wanaotaka kuzungumza chochote maana kila mtu amejaliwa mdomo wake wa kusema,” alisema Petit Man