KOCHA aliyesitishiwa mkataba wake Simba SC, Mrundi Masoud Djuma amesema anaamini ipo siku atarejea tena kukinoa kikosi hicho cha wekundu wa msimbazi kwa sababu ameondoka akiwa hana ubaya na uongozi wake.

Djuma ambaye amesitishiwa mkataba wake baada ya kushindwa kuelewana na kocha mkuu, Patrick Aussems ambapo sasa anatajwa kujiunga na kikosi cha African Lyon.

Kocha huyo anaondoka leo kurudi kwao Burundi kwa usafiri wa gari lake mwenyewe baada ya kukamilishiwa kitita chake cha Milioni 17 kama kifuta jasho baada ya mkataba wake kusitishwa.

” Nimeachana na Simba vizuri, nawatakia kila la heri katika michuano yote ambayo Simba inashiriki msimu huu, mashabiki na wanachama wake wamekuwa na mapenzi makubwa na mimi, sina tatizo nao na ninaamini ipo siku nitarejea,” amesema Djuma.