Alikiba aeleza ni kwanini MoFaya haijaingia sokoni

Msanii wa muziki Bongo, Alikiba amefunguka kwanini hadi sasa kinywaji chake cha MoFaya hakijaingia sokoni.

Muimbaji huyo amesema kila hatua imekamilika ingawa kuna kitu kilikwambisha ila ana imani siku sio nyingi kitaingia sikoni.

“Ok, tayari tumemaliza kila process nadhani kuna delay kidogo imetokea ambayo imefanya hadi sasa watu hawaioni katika soko ila bila shaka Mwenyenzi Mungu akijali hivi karibuni itakuwa tayari na ninaomba Watanzania waipokee,” Alikiba ameiambia Utakumbuka kinywaji cha MoFaya kilitambulishwa kwa mara ya kwanza April 29, 2018 ambayo ilikuwa siku ya harusi ya Alikiba.