Harmonize Aimwagia Mamilioni Timu ya Ndanda Fc Baada ya Kukwama Hotelini

Msanii wa bongo fleva Harmonize ambaye pia ni shabiki mkubwa wa timu ya Ndanda SC, ametoa shilingi milioni 3.5 kwaajili ya kuisaidia timu hiyo iliyokwama mkoani Singida baada ya mchezo wake wa LigikuuTanzaniaBara uliochezwa Oktoba 6, 2018 dhidi ya Singida United, na kufungwa mabao 3-1.

Timu hiyo ilizuiwa kuondoka baada ya kushindwa kulipa gharama za hotel pamoja na kukosa nauli ya kurejesha mkoani Mtwara.

Ndanda SC wamemshukuru muimbaji huyo ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani kwaajili ya show za tour yake ya kimuziki.