Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva aliyewahi kutamba miaka ya nyuma Q-Jay ameibuka na kukana vikali taarifa zilizoenea Kwenye mitandao ya kijamii kuwa amerukwa na akili.

Taarifa Hizi zilisambazwa na msanii mwenzake anayejuliaka kama Makamua ambaye aliwaomba Watanzania wamchangie Q- Jay kwa madai ameathirika na madawa ya kulevya kiasi cha kuanza kuokota makopo.

Baada ya kusambaa kwa taarifa hizo Q Jay ameibuka na kuzikana vikali ambapo Kwenye mahojiano aliyofanya kituo kimoja cha habari amefunguka haya:

Habari hizo sio za kweli ila kitu kilichotokea ni kwamba nilipitia changamoto fulani Kwenye maisha lakini sio kwamba nilikuwa Chizi naamini hata wewe mwenyewe unaweza ukaona kuwa Chizi hawezi kuongea kama mimi”.

Lakini pia Q- Jay amelaani matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na kudai taarifa hiyo ilikuzwa kutokana na watu kutumia mitandao ya kijamii vibaya: