Msanii wa Bongofleva, Alikiba maarufu kama ‘King Kiba’, amechoshwa na usumbufu wa habari zinazosambaa kuwa mke wake ana ujazito na ameamua kuweka wazi kuwa mke wake hana ujauzito.

Pia amefunguka kuwa tangu amefunga ndoa amebadili tabia yake na kwa sasa anamuheshimu sana mke wake, lakini pia usumbufu wa wanawake kumtongoza mitandaoni  umepungua sana kwa kuwa wanajua kaoa.

“Kuna taarifa niliziona mitandaoni zikisema kwamba mke wangu ni mjamzito lakini taarifa hizo sio za kweli, kwenye ile picha mke wangu alikuwa amevaa koti langu ambalo lilitunishwa na upepo ikaonekana kama mjamzito lakini hana mimba na yupo sawa”, amesema Alikiba.

Kiba ameiambia eNewz ya  kuwa kwa sasa amekuwa akijiheshimu na kumuheshimu mke wake tofauti na alivyokuwa kipindi hajaoa, ambapo wasichana walikuwa wakimsumbua kwa wakidhani yakwamba wanaweza kupata nafasi ya wao kuolewa kitu ambacho sasa hakipo kabisa.

Pia Kiba alimalizia kwa kusema kwamba haongozani na mke wake mara kwa mara kwa kuwa mke wake ni msomi ambaye yupo ‘busy’ na kazi zake, lakini pia mke wake sio mtu wa kupenda kuonekana  na hapendi umaarufu kwa ujumla ndo maana anaweza akawa naye sehemu mbalimbali lakini asijionyeshe mbele za watu.