NAIBU Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile kesho kutwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa fursa kwa wanamuziki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk.Donald Kisanga alisema mkutano huo ni muhimu sana kwao.

“Mkutano huu utakaofanyika kesho kutwa ni muhimu sana kwetu kwani utawakutanisha wanamuziki mbalimbali hivyo ni vema wanamuziki wakajitokeza” alisema Dk.Kisanga.

Dk.Kisanga alisema katika mkutano huo Ndugulile atapata fursa ya kugawa kadi za matibabu za mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) katika ukumbi wa NSSF Ilala.