Shonza Kula Sahani Moja na Sister Fey

Mh naibu waziri wa sanaa na michezo bado  anaendelea kupigilia msumari wa moto na kufuatilia mienendno ya mwanadada Sister Fey kutokana na tabia yake ya kuwa anafabya mambo yanayowakwaza watu hasa baada ya kujiingiza katika mahusiano na kijana anaemzidi umri.

Mh Juliana Shonza haitakuwa mara yake ya kwanza au ya pili kujaribu kumuonya msanii huyo kuwa na nishamu na kuangalia kitu cha kuposti katika akaunt yake ya instagram kwa sababu vingi anavyoviweka haviedani na maadili ya sanaa.

Kama inakumbukwa siku chache za nyuma, msanii huyo aliwekwa ndani kwa kauli ya mh naibu waziri  baada ya kuweka picha chafu akiwa na mume wake huyo katika mitandao.

Akizungumza na wageni waalikwa katika party ya ACTWITHMONALISA , Mh naibu waziri anasema “wakina sister fey wanajifanya kuwa wao ni wasanii wakati wanafanya vitu vya ajabu katika mitandao wanadhallisha sana tasnia ya sanaa.