Msanii wa bongo fleva, Hytham Kim ambaye hivi karibuni aliweka picha mtandaoni ikimuonesha akiwa mjamzito, amejibu tuhuma hizo, akisema kuwa kitendo hicho ni cha kawaida.
Hytham amesema kitendo hicho ni kitu cha kawaida, hivyo hajali watu wanaosema nini juu yake kwani yeye sio wa kwanza.
“Ni kawaida sioni cha ajabu kwa sababu lile ni tumbo tu, kila mtu ana tumbo isipokuwa utofauti ni kwamba lile limebeba mtoto, sioni cha ajabu sana, wapo wabongo waliowahi matumbo yao wakiwa na ujauzito mimi sio mtu wa kwanza, kila mtu ana utamaduni wake na mfumo wake wa kuishi, kwangu mimi sioni kitu cha ajabu”, amesema Hytham.
Msanii huyo amepost picha ya tumbo lake akiwa mjamzito, hali iliyopelekea watu kumjia juu kuwa picha hiyo haipendezi usoni mwa jamii.