Aika Atoa ya Moyoni Kuhusu Skendo za Daimond na Hamissa Mobeto

NAVY KENZO moja kati ya makundi bora kuwahi kutokea kunako Muziki wa Bongo Fleva, miaka miwili ya nyuma kundi hili ambalo linaundwa na kapo, Aika Marealle na Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ lilikuwa ‘hot’ na baada ya hapo likazima ghafla huku chanzo kikitajwa kuwa ni likizo ya uzazi baada ya Aika kujifungua.

Kwa sasa limerudi tena likiwa juu na ngoma yao ya Katika wakimshirikisha mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Mikito Nusunusu limefanikiwa kukutana na Aika ambaye amefunguka mengi kuhusiana na maisha yake na muziki kwa ujumla, huyu hapa;

Mikito Nusunusu: Kitu gani ambacho utakikumbuka kutoka kwa Prodyuza Pancho Latino aliyefariki hivi karibuni?

Aika: Pancho ni jina kubwa na kajitahidi kufanya vitu vikubwa kwenye soko la muziki siyo mimi tu nitakaye mkumbuka hata Watanzania watamkumbuka kwa mengi mno kwa sababu ana mchango mkubwa sana kwenye gemu ya Bongo Fleva.e

Mikito Nusunusu: Muziki unaathiri malezi ya mtoto yako?

Aika: Hapana, kila kitu nimekipangilia, nimebalansi kote nimehakikisha malezi ya mtoto nayafanya inavyotakiwa bila kisingizio cha kazi zangu za muziki.

Mikito Nusunusu: Una mpango wa kuja kuongeza mtoto mwingine hivi karibuni?

Aika: Ndio! Hata mia yaani maana napenda sana watoto (anacheka).

Mikito Nusunusu: Kuna mistari ambayo ameimba Diamond mwishoni katika wimbo wenu wa Katika, amemtaja Hamisa Mobeto imekuwa gumzo sana vipi mashabiki hawajawashambulia kuwa mnamuunga mkono Diamond?

Aika:Hapana! Tena huo ndio ubunifu ambao unatakiwa katika muziki maana kitu kinapokuwa kinaongelewa halafu ukakiweka katika muziki ili kuburudisha watu inakuwa sio kitu kibaya sisi tuliona kawaida na ni njia ya kufanyabiashara na nina uhakika hata muhusika mwenyewe alipokisikia alikifurahia.

Mikito Nusunusu: Ushawahi kuwa na mawasiliano na Hamisa?

Aika: Ndio nachati naye sana tu!

Mikito Nusunusu: Unapokuwa na shoo au safari za nje ni vitu gani ambavyo huwa unafanya ili kuhakikisha kwamba mtoto anabaki salama?

Aika: Nimemchukua mdogo wangu nipo naye pale nyumbani, ili kuhakikisha kwamba hata kama kuna kina dada (wafanyakazi wa ndani) lakini mdogo wangu awepo pale anamuangalia.

Mikito Nusunusu: Diamond ni mtu ambaye mnafanya naye kazi mmeshawahi kukaa naye mkamshauri kuhusu hizi skendo zake za wanawake kila siku mitandaoni?

Aika: Hapana! Mimi huwa siwezi kumhukumu mtu na maisha yake na kila anachoamua kukifanya, ila ni mtu ambaye nimekaa na Diamond kwa nyuma ya pazia ambapo naona jinsi anavyoishi na watu vizuri, hao wanawake wote mnaosema anawadhalilisha anaishi nao vizuri na anawajali.

Mikito Nusunusu: Vipi kuhusu ndoa yenu?

Aika: Sidhani kama ndoa ni kitu cha lazima sana maana mimi na baba mtoto wangu tunaishi kama mtu na mume wake na kuna muda tunaona kama tumeshafunga ndoa.