Image result for Tiko Hassan

Msanii wa filamu ambaye kwa sasa anafanya bongofleva, Tiko Hassan, amefungukia kauli ya Ray C aliposema watu wengine sio lazima nao wawe wasanii, kwani hawana uwezo wa kuimba vizuri.

Tiko amesema kwamba Ray C hana mamlaka ya kumhukumu mtu juu ya uwezo wake wa kuimba, isipokuwa kama mtu anajiamini basi anaweza kufanya hivyo.

“Mimi naamini kila mtu anaweza kuimba, ‘as longer as’ anajiamini anaweza kufanya, yeye nani ‘ajudge’ mtu mwingine!” amesema Tiko Hassan.

Hivi karibuni baada ya mwanamitindo maarufu bongo Hamisa Mobetto kuachia wimbo wake mpya, Ray C aliibuka na kumshutumu kuwa hajui kuimba na kusema kwamba sio lazima kila mtu aimbe.