Taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusu Petitman Wakuache kufunga ndoa na mwanamke mwingine siku ya October 12,2018 ikiwa bado Mwanamke huyo hajafahamika.

Tetesi hizo zimeanza kusambaa baada ya Petitman Wakuache kupost picha kupitia ukurasa wake wa instagram akionekana anafunga ndoa na kuandika neno ‘Alhamdulilah’. Inasemekana pia ndoa hiyo imefungwa maeneo ya Manzese Big Brother.

Inasemekana kuwa Petitman anaweza akawa amefunga ndoa na Mnyarwanda ambaye alichukua headllines siku kadhaa zilizopita kwenye mitandao ya kijamii baada ya kudaiwa kuwa ndio mpenzi mpya wa Petitman Wakuache.