Chid Benz Amtupia Lawama Jux

MSANII wa Muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro maarufu kama Chid Benz amefungukia madai ya kufanya shoo ya msanii mwenzake Juma Jux iliyoitwa Money & Love kisha kutolipwa baada ya ku-perform.

Chid amedai kuwa Jux ni msanii mzuri na anamkubali sana tu, lakini alichokifanya si sahihi na kusema kuwa yeye ni mmoja wa wasanii ambao wanawasaidia wasanii wenzake licha ya baadhi yao kutoona umhimu wake na mchango wake katika game ya Bongo Fleva.