go, Irene Uwoya, hivi karibuni imekuwa ikisemekana amechachana na mume wake, msanii Dogo Janja na kuolewa na mwanaume mwengine kimya kimya.

Irene Uwoya amefunguka juu ya ndoa hiyo ya pili, na kusema kwamba hakuna ukweli wowote juu ya tetesi hizo.

“Hapana, hakuna kitu kama hicho, mimi nilikuwa kwenye sherehe jana, kwanza siwezi kuongelea mambo yangu ya hivyo, labda kama kuna kingine”, amesema Irene Uwoya.

Hivi karibuni kuliibuka tetesi kwamba msanii huyo ambaye kwa sasa hivi anatikisa mitandao ya kijamii kwa kupendeza, ameachana na mume wake Dogo Janja, na kuolewa na mfanyabishara mkubwa  aliyejulikana kwa jina la ‘Salaah’, ambaye amechora tattoo yake.