Muimbaji wa zamani wa muziki wa Taarabu, Alhaji Mzee Yusuf usiku wa kuamkia leo amefiwa na mama yake mzazi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mzee Yusuf amethibitisha taarifa hizo kwa kuandika “Qalu inna lillah wa inna ilayh rajiunna. Mama yangu mzazi hatunae mda huu Allah anijaalie nguvu za kusimama na kufika znz asubuhi. Amiin usiku huu utakua mrefu sana leo lkn tuseme tena inna lillah wa inna ilayh rajiunna. Allah ampe qauli thabit mama yangu kipenzi. Amiin.“.