Msanii wa miondoko ya HipHop nchini Rashid Makwiro maarufu Chid Benz amemshtumu msanii wa Bongofleva Jux kwa madai ya kutomlipa katika ‘show’ ya Money & Love iliyoandaliwa na Jux pamoja na Vanessa.

Chid Benz amesema Jux ni moja ya wasanii wenye heshima na anao wakubali nchini, lakini hakupendezwa na kitendo alichokifanya cha kutompatia chochote, huku akisema yeye ni moja ya wasanii wanaotoa msaada kwa wasanii wenzake licha ya baadhi kutoona umuhimu na mchango wake katika ‘game’ ya Bongofleva.

“Jux hakutoa chochote kile, mimi silii kwamba Jux anilipe hela, lakini heshima ndio kitu kikubwa, haijalishi kwamba nilikua kwenye listi ya wanaotumbuiza au sikuwepo ila ishu nzima alipanga kwasababu alijua nikimpandisha Chid ‘stejini’ watu wataonesha upendo mkubwa kwangu na kutachangamka, lakini yote niliyoyafanya alishindwa hata kusema kaka hiki hapa kifuta jasho”, amesema Chid Benz.

Kuhusiana na ‘issue’ ya wasanii wa sasa kutowaheshimu wasanii wa zamani Chid Benz amesema,

“heshima imepungua kwa baadhi ya wasanii kabisaa wa bongo fleva nchini wapo ambao wakiniona wananisalimia na kuniamkia kama Barnaba, Linah, ni wasanii wenye heshima, tatizo lake Jux ni kutonilipa pesa zangu hakuna mtu ambaye alienda ‘kushow love’, ‘show’ ilipangwa na akatangaza kwamba nitapanda stejini lakini anashindwa kunipa changu”.