ally-hapi-29

MKUU wa  mkoa wa Iringa Alli  Hapi  ameombwa  kuwawajibisha  watendaji  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa    waliopuuza  agizo la  ofisi ya mkuu  wa  mkoa  iliyotolewa na  aliyekuwa  mkuu  wa mkoa wa Iringa Amina Masenza  kuhusiana na mgogoro wa mpaka kati ya  Manji na  Cosmas Msigwa .

Akizungumza na mtandao huu  leo  Jamila Manji  amesema  kuwa    kufuatia  mgogoro  huo  wa  mpaka  uliokuwepo  eneo la  kiwanja   kilichopo  eneo la  stendi  kuu ya  mkoa wa Iringa  ofisi ya  mkuu wa  mkoa wa Iringa chini ya  aliyekuwa  mkuu wa mkoa  Amina Masenza  ilitoa majibu kwa barua   tarehe 27/6/2018 .

Kuhusiana na  jinsi ambavyo  ofisi ya  mkoa  ilivyoweza  kushughulikia  mgogoro  huo   kuwa  baada ya  ofisi ya  mkuu  wa mkoa kupokea malalamiko hayo  ilituma  timu ya  wataalam  ili  kupata  ukweli  wa mgogoro huo na  kutafuta  suluhu ya  kudumu .

kuwa  wataalam  wamepitia  nyaraka zote  zinazohusiana na suala  zima la ujenzi  ndani ya Manispaa pamoja na  kutembelea eneo husika kuchukua  vipimo  na  baada ya hapo  walibaini  kuwa ujenzi wa msajengo hayo  mawili katika mpaka unaotenganisha  haukufuata vipimo kama sheria inavyoelekeza .

Hivyo kutokana na  kulifanyia kazi  suala hilo ofisi ya  mkoa  ilitoa  maelekezo  likiwemo la Transfoma iliyowekwa  kwenye hifadhi ya  barabara ‘Road Reserve’ ambayo imeziba  uchochoro uliopo kati ya nyuba hizo  kwa  maana ya Manji na  Msigwa  ihamishwe kwenye  eneo hilo  la uchochoro ili  kuruhusu matumizi halali  ya uchochoro  huo .

Kuwa  jukumu la  kusimamia  zoezi hilo  walipewa  TANESCO na ofisi na  mkuu wa mkoa na Hlamashauri ya  Manispaa ya  Iringa  chini ya  mkuu wa wilaya ya  Iringa .

Amesema  Manji  kuwa  jukumu  jingine  kupitia maagizo yaliyotolewa katika barua  hiyo na ofisi ya  mkuu wa mkoa ni uchororo   kuachwa  mita 1.5 kila  upande  kwa  mujibu wa  sheria  ya  mipango  miji  sura  355 kifungu  77(i) na kanuni  zake za  mwaka 2011 kama  zilivyotanganzwa  kwenye gazeti la  serikali  Na 395 la  tarehe 2/12/2011 na  jukumu  la utekelezaji  lilikuwa  pande  zote  mbili  tuliokuwa  tunavutana.

Pamoja na maagizo hayo ya  ofisi ya  mkuu  wa mkoa bado amedai kuna  upuuzwaji mkubwa kwani Transfoma hiyo badala ya  kuhamishwa  imeshushwa  chini  pia  ujenzi  wa  eneo la uchochoro  huo  limeanza  kufanyika  toka  ijumaa wiki  hii  kinyemela bila  mgogoro  huo  kufikia suulu  .

Manji  amesema  kwa  kuwa  amepata  kufika  ofisi  ya Manispaa  na  kumtafuta mkurugenzi a  kumkosa  bado kaimu  mkurugenzi  simu yake  hakuweza  kupokea  ijumaa hadi  saa 10 jioni na  ofisi ya  mkuu wa  mkoa   kwa sasa ni  tegemeo lake kubwa kwani wananchi wanyonge wa Iringa  wanaimani  kubwa na hatua ya  Rais Dkt  John Magufuli  kumteua na  kumleta  mkoa wa Iringa Alli  Hapi  kwani anaamini ni  ukombozi wa  wanyonge na  suala lake anaomba lifanyiwe kazi .