Breaking News: Familia ya Mo Dewji Yatangaza Kutoa Bilioni Moja kwa Atakayetoa Taarifa Wapi Alipo Mo

Familia ya Dewji imetangaza zawadi ya Tsh. Bilioni Moja (1,000,000,000) kwa mtu yeyote ambaye atatoa taarifa ambazo zitawezesha kupatikana kwa Mohammed Dewji.

Kauli hiyo imetolewa hivi punde na familia ya Mo Dewji wakati ikizungumza na waandishi wa habariĀ katika ofisi za kampuni ya MeTL Group zilizopo katika jengo la Golden Jubilee TowersPosta jijini Dar es Salaam.

Mwenye taarifa anaweza kuwasiliana na mwanafamilia Murtaza Dewji kwa namba 0755030014, 0717208478, 0784783228 na email ya findmo@metl.net