Beki kiraka wa Simba, Erasto Nyoni ameongezwa katika kikosi cha Taifa Stars.

Nyoni atakuwa katika kikosi cha Taifa Stars kitakachoivaa Cape Verde katika mchezo wa marudiano utakaopigwa kwenye dimba la Taifa kesho Jumanne.

Nyoni amekuwa hakosekani kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania kwa kipindi cha miaka 10 sasa tangu alipofunga goli pekee katika ushindi wa bao 1-0 ambao Stars iliupata ugenini dhidi ya Burkina Faso mwaka 2008.

Kocha Emmanuel Amunike ameamua kuongeza nguvu ya kiungo chake cha ukabaji ambacho kina pengo kwa kuwa Jonas Mkude pia ni majeruhi.