Esma Ajiweka Pembeni na MAMA yake Bi Sandra

DADA wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Khan amefungukia ishu ya yeye kuwa mshauri wa mama yake, Sanura Kassim ‘Bi Sadra’ na yote anayoyafanya mitandaoni na kusema amejitoa rasmi.
Esma aliiambia Over Ze Weekend kuwa, kwa sasa amejitoa rasmi kuwa mshauri wa mama yake huyo.
“Nilikuwa ninampa ushauri kama mwanaye maana mimi ndiye mtoto wake mkubwa, lakini kwa sasa mama ana mume wake ambaye ni Anko Shamte kwa hiyo ndiye mshauri wake, sisi tunakaa pembeni,” alisema Esma.