Jaji Mkuu Amtembelea Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ofisini Kwake

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma  amefanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella, nakupata wasaa wa kutoa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na wananchi wote waliopatwa na maafa ya kivuko cha MV Nyerere yaliyotokea Septemba, 20, 2018 katika wilaya ya Ukerewe.

Aidha; Mhe. Jaji Mkuu alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ushirikiano katika ya ofisi yake na Mahakama mkoani humo.