Siku moja iliyopita msanii wa Bongo Fleva, Hawa alisafirishwa kuelekea nchini India kwa ajili ya matibabu ya maradhi yaliokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu.

Hawa alijizolea umaarufu mkubwa aliposhirikishwa na Diamond Platnumz kwenye wimbo wake uitwao Nitarejea uliyotoka mwaka 2010 nchini ya Producer Bob Junior ndani ya studio za Sharobaro Records.

Baada hapo hakuweza kusikika akifanya vizuri zaidi kwenye wimbo mwingine hadi pale zilipoanza kuchipuka kwa taarifa kuwa muimbaji huyo ametumbukia kwenye matumizi ya dawa za kulevya kitu kilichoipa famili yake mzigo mkubwa wa matibabu.

Kwanini Diamond

Wakati Hawa amekuwa mgonjwa, Diamond Platnumz alikuwa akinyooshewa kidole kutokana alionekana ndiye mtu pekee mwenye uwezo wa kumsaidia kutokana na ukaribu wao hapo awali na kazi walizofanya.

September 28, 2018 Diamond alichapisha ujumbe kwenye ukarasa wake wa Twitter kueleza kuhusu mpango wake ya kumsaidia Hawa.

“Nipo namshughulikia now kwenda India kutibiwa ila sikutaka kutangaza kwa  staki watu wachukulie msaada wangu ni kiki but kwakuwa maswali yamekuwa mengi juu yake, imebidi nijibu na matibabu yake si chini ya milioni 50 na nitadeal nayo tu,” alieleza Diamond.

Babu Tale ambaye ni Meneja kutokea WCB kwenye mahojiano na Wasafi TV alisema alipewa taarifa na Diamond akiwa kwenye show nchini Namibia na kumuelekeza kufuatilia suala la Hawa.

“Nilishakutana naye mara mbili nikamwambi siku moja ukijisikia kubadilika njoo tusaidiane hatuna uwezo mkubwa lakini tutasaidiana kupitia hapo,” alisema Babu Tale.

Hadi sasa Hawa anapatiwa matibabu nchini India, pia katika safari yake aliongozana na mama yake mzazi. Hivyo Diamond Platnumz ametekeleza kile alichohaidi hapo awali.

Kwa mujibu wa taarifa ya awali matibabu ya hawa yatagharimu takribani Tsh. Milioni 50. Pia utakumbuka October 05, 2018 wakati akiwa nyumbaji kwao Tandale alitoa msaada kwa watoto 300 ambao walipatia bima ya afya, mitaji ya biashara kwa kina mama 200 pamoja na Bodaboda 20 kwa vijana.