Mwakasege Afunguka Kuhusu Kifo cha Mwanaye

HATIMAYE Mchungaji Mwalimu Christopher Mwakasege amefunguka kuhusu kifo cha mwanaye wa kiume Joshua ambaye alifarikiAlhamisi iliyopita, majira ya saa 2, usiku lakini taarifa hizo zilikuwa hazijathibitishwa na mtu yeyote kutoka ndani ya familia na mchungaji huyo alikuwa akiendelea na Semina yake.

“Alhamisi usiku tulifiwa na mtoto wetu Joshua, alifariki ghafla, halikuwa jambo jepesi kwamba tuendelee na semina au tusiendelee, kwa jinsi ya binadamu halikuwa jambo rahisi kuendelea na semina. Biblia inatuambia tuwe tayari wakati unaofaa na usiofaa.

“Kwa jinsi ya kibinadamu kipindi hiki sio wakati unaofaa kuendelea na semina lakini kwa Mungu yeye anajua. Niliwaomba ndugu zangu niendelee na Semina wakaniuliza una nguvu za kuendelea nikawaambia niombeeni tu! Mungu atanisaidia,” alisema Mwakasege.