Mwana FA Atoa ya Moyoni ''Wenzenu mnatukwaza kwelikweli''

Mkali wa HipHop Bongo, Mwana FA, amewachana mashabiki wake kuwa wanamkwaza kwelikweli kwa kuandika ‘comment’ za matangazo kwenye ‘post’ zake anazoweka kwenye mtandao wa Instagram.

Kupitia ukurasa wake wa ‘Instagram’ Mwanafalsa amedondosha ujumbe mzito ambao ameeleza kuwa umetoka rohoni mwake, huku akiambatanisha picha mpya ambazo zinaonesha sio mazingira ya kawaida na kudhaniwa ni ‘Location’ ya ‘video’ yake mpya.

Wiki hii mpya ndugu zetu wa matangazo tunawaomba,tupo chini ya miguu yenu,tusameheni,msiweke matangazo yenu kwenye posts zetu..kwa hisani yenu,mnatukwaza kwelikweli wenzenu hivoo.. Ama baada ya maombi hayo yaliyotoka rohoni kabisa,tuseme tangazo moja block moja,sawa?..wasalaam..nawaombea wiki njema.

Picha hizo zimemvutia ‘producer’ wa ‘show’ kubwa ya muziki nchini, Planet Bongo ya East Africa Radio, Grayson Gideon ambapo moja ameiita kama picha ya siku ya leo huku akiweka wazi kuwa hadhani kama kuna ujio mpya wa msanii huyo kwani hiyo sio dalili ya Mwana FA kuachia ngoma.

Hata hivyo mashabiki wake wamemcharukia staa huyo kwa kumwambia waondio wamemuongezea idadi ya wafuasi mitandaoni, hivyo anavyowazuia kutangaza biashara zao nao wanaweza kuamua kutomfuata na mwisho wa siku hatakuwa na wafuasi.