Mwanadada Diva the Bawse aamefunguka na kusema kuwa amethitisha swala la kuomba msaada kwa ajili yya kupta pesa hizo li aweze kuzitumia kwenda hospitali na kuonana na wataalamu watakaomsidia kupata mimba kwa kutumia njia ya IVF.

Miezi michache iliyopita, mwaadada Diva the bawse alifunguka na kuwaambia mashabiki kuwa alipata daktari mtaalamu wa mambo ya wanawake na kumwambia kuwa kwa jinsi ali ilivyo sasa hawezi tena kuzaa au kupata mimba kwa njia ya kawaida labda kufanyiwa matibabu na kupandikizwa mbegu lalkini sio kwa njia ya kawaida.

Hata hivyo alianza kuwaomba amshabiki kumchangia kidogo walichonacho ili aweze kukamilisha zoezi ilo lakii ghafla amebadilisha msimamo wake na kusema ameona kuwa ni bora swaa hilo libaki kuwa la kwake mwenyewe bila kuwaomba msaada mashabiki zake.

Nimesitisha kuchukua michango, nimeona kuwa ni bora swala hiloliwe la kwangu mwenyewe,hivyo nina bajeti yangu rayari ninasubiri muda muafaka tu ufike , naamini na mimi nitaitwa mama.