Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ametuma salama za rambirambi kwa Rais wa Uganda Museveni kufuati vifo vya waganda 40 vilivyosababishwa na maporomoko ya udongo

Rais Magufuli ameandika katika twitter yake “Nakupa pole Rais Museveni na wananchi wote wa Uganda kwa kuwapoteza watu zaidi ya 40 katika ajali ya maporomoko ya udongo iliyotokea katika Wilayani Bududa. Watanzania tunaungana nanyi katika kipindi hiki cha majonzi na tunawaombea majeruhi wote wapone haraka”