Wanaotaka Nishuke Watasubiri Sana :-Riyama Ally

Mwanadada Riyama Ally kutoka kwanda cha filamu nchi amaewapa pole sana wale wanaokaa na kumuomba mabaya kwamba hana muda mrefu sanaa yake na kipaji chake kitashuka na jina lake halitakuwepo tena katika tasnia ya filamu nchini,.

Riyama ambae amekuwa moja ya wasanii wa kike wenye kipaji cha hali ya juu na kupendwa sana na watu kwa sababu ya kazi zao anasema kuwa wapo watu wanamuombea kushuka kwa kipaji chake lakini yeye anaamini kuwa mungu anamuongoiza hivyo hakuna linaloweza kuharibika.

Kwa wale wanaosubiri kushuka kwangu watasubiri sana,  kwa sababu kushuka kwangu ni ngumu sana  sitashuka mpaka uzeeni nitakuwa bora zaidi.

Riyama pia amewataka wasanii wenzake kuwa wakweli kila mara hasa wanapokuwa wanaulizwa juu ya wale waliowashika mkono na kuwavuta mpaka kufikia pale walipo.