Wafanyabiashara wakubwa wapewa angalizo

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Kangi Lugola, jana awataka wafanyabiashara wakubwa na watu maarufu kuwa makini na suala la ulinzi wao binafsi.

Kwa mujibu wa Spoti Xtra, Lugola alisema hayo kutokana na tukio la kutekwa kwa Mfanyabishara kijana na bilionea, Mohammed Dewji ‘Mo’ akieleza kuwa ni muhimu kwa usalama wao.

“Suala la kujihakikishia usalama binafsi ni jambo muhimu sana kwa hawa watu,”alisema Kangi ambaye ni Mbunge wa Mwibala tangu mwaka 2010.

Mashabiki hususani wa Simba wamekuwa wakijiuliza kuhusiana na kama MO alikuwa na ulinzi binafsi au la ingawa habari za awali zinadai kwamba alivyotekwa hakuwa na mlinzi alikuwa mwenyewe.

Kauli hii ya Lugola ina maanisha kuwa matajiri wengine wakubwa hapa nchini akiwemo Yusuf Manji ambaye amewahi kuwa mfadhili na kiongozi wa Yanga wanatakiwa kujiwekea ulinzi wa kutosha ili kuepuka kukumbwa na hali kama hii ya Mo.