Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetokea katika kundi la Navykenzo, Aikah Marealle ambaye hivi sasa pamoja na mpenzi wake Nahreel wanafanya vizuri na ngoma yao ya ‘Katika’ amefunguka na kumuongelea Diamond Platnumz.

Aikah na Nahreel wameonekana kuwa na ukaribu mkubwa na Diamond hii ni baada ya kumshirikisha katika ngoma yao ya Katika lakini kuna tetesi zilisambaa kuwa kundi hilo Lina mpango wa kusainiwa chini ya WCB tetesi zilizokataliwa na Navykenzo.

Lakini pia siku za hivi Karibuni Diamond amekuwa akinyoshewa sana vidole kwa tabia yake anayo tuhuma ya kumdhalilisha wanawake ambapo mashabiki walimjia juu kwa vitendo ambavyo vilimuonyesha kama hawaheshimu wanawake waliomzalia ambao ni Mobetto na Zari.

Aikah alihojiwa kuhusu tuhuma hizo za Diamond kudhalilisha wanawake ambapo alifunguka kwa kusema:

Mimi huwa siwezi kumhukumu mtu na maisha yake na kila anachoamua kukifanya, ila ni mtu ambaye nimekaa na Diamond kwa nyuma ya pazia ambapo naona jinsi anavyoishi na watu vizuri, hao wanawake wote mnaosema anawadhalilisha anaishi nao vizuri na anawajali“.

Lakini pia Aikah aliulizwa kuhusu mstari ambao umesikika Kwenye wimbo huo ambapo Diamond alimtaja Hamisa kuhusu uchawi na matunguli:

Tena huo ndio ubunifu ambao unatakiwa katika muziki maana kitu kinapokuwa kinaongelewa halafu ukakiweka katika muziki ili kuburudisha watu inakuwa sio kitu kibaya sisi tuliona kawaida na ni njia ya kufanyabiashara na nina uhakika hata muhusika mwenyewe alipokisikia alikifurahia”.

Aika amesisitiza kuwa hana tatizo na Hamisa na ni mtu wake ambaye anachat naye mara kwa mara.