Chidy Benz Achimba Mkwara Mkali ''Ukifuatilia maisha yangu ntakuzibua''

Msanii wa muziki wa HipHop nchini, Rashid Makwiro maarufu ‘Chid Benz’ amesema amechoshwa na watu wanaomkebei kuhusiana na kukonda kwake na kuwataka wafatilie maisha yao.

Chid Benz amesema kauli za watu wa mitandao zimekuwa zikimuandama juu hali yake kiafya ikiwa pamoja na Kukonda kwake huku wengi wakimshtumu kutumia madawa ya kulevya bila kujua kwamba hali ya hewa ndio iliyomfanya apungue.

“Nawashangaa wanaosema nimebadilika,mimi nipo vilevile, mi nahisi nimebadilika kwa watu wachache wasionijua vyema, mimi nimebadilika nini, umbo au?, familia na watu wangu wanajua kwamba nilizaliwa nikiwa mwembamba, mziki ukanipa pesa nikanenepa nikawa na misuli lakini badae hali ya hewa ikanibadilisha, mbona Peter Msechu hakuanza na tumbo lake alilonalo sasahivi, lakini hali ya hewa imenibalisha”, amesema Chid Benz.

Kuhusiana na tuhuma anazotupiwa na mashabiki mitandaoni kuwa anatafuta kiki ya kurudi kimuziki chibenz amewaonya mashabiki wanaomfatilia mitandaoni kuacha tabia hiyo.

“Hao watu mnaowaona wanatoa komenti ni watu wa watu,wanafungua akaunti kwa ajili ya kutukana watu,kurushia watu maneno na kuwarudisha nyuma, mimi msinifanyie michezo hiyo, maana mitandao yenyewe sikuizi wanaonesha mtu yuko wapi, hata ukiwa Tabata au uchochoroni ntakufuata ntakuzibua, bora nipoteze muda wangu kuwafundisha watu adabu kuliko kukaa maskani kupoteza muda”, ameongeza.

Siku za hivi majuzi Chid Benz amemshutumu msanii wa Bongofleva Jux kwa madai ya kutomlipa pesa zake katika ya show ya Money & Love iliyoandaliwa na Jux pamoja na Vanessa.