Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameibuka na kumuomba msamaha Msanii mwenzake Shilole baada ya bifu la muda mrefu.

Bifu la Shilole na Gigy Money liliwahi kutawala vichwa vya habari siku za nyuma ambapo Gigy Money alimtolea povu Shilole na kuponda muziki wake na kudai hajui kuimba Lakini pia aliponda kingereza chake anachoongea.

Lakini baada ya miaka kadhaa kupita tangu sakata hilo hatimaye Gigy Money amemuomba radhi Shilole Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amemshukuru kwa mchango wake na kumpa ushauri wa kumlea mtoto wake kama mama.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Gigy Money ameandika:

Miaka michache nyuma mimi nilikuwa namuongelea vibaya shishi bila kujali ni mama au ana mawazo gani kwa wakati ule basi leo nachukua nafasi hii kumwambia samahani Dada Shilole kwani sikua najua kama na mimi ntakuwa mama au nilikuwa najiona keki kumbe maandazi”.

Hivi sasa Gigy Money ni mama wa mtoto mmoja wa kike anayeitwa Mayra aliyezaa na aliyekuwa mpenzi wake Mo J.