“Siwezi Kusaidia Yatima Wakati Familia Yangu Maskini”-Gigy Money

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi kuwasaidia watoto yatima ilihali familia yake pia inahitaji msaada kutoka kwake.

Kwenye mahojiano na kitu kimoja habari, Gigy Money aliulizwa endapo ana mpango wa kufanya shughuli za kijamii ikiwemo kusaidia watoto yatima lakini Gigy Aliweka wazi kuwa hana Mpango wa kufanya hivyo.

Siwezi kusaidia watoto yatima kabisa! Sio kwamba sipendi kusaidia ila mimi mwenyewe Familia yangu ina mayatima wengi na siku za nyuma nilikuwa naenda kutoa Misaada lakini sasahivi nimekuwa najiangalia ndugu zangu kibao wamekufa wameacha mayatima hawana mtu wa kuwasaidia inabidi nifocus Kwenye Familia yangu kwanza mambo yakikaa vizuri ndio niweze kusaidia watu wa nje”.

Lakini pia Gigy Money amesisitiza kuwa hawezi kutoa Misaada kwa nia ya kujionyesha kwa Watu ili waone kweli anatoa halafu watu katika familia yake hawana msaada.

Mashabiki wengi wampongeza Gigy kwa Kauli yake na kuwataka wasanii waache unafiki wa kutoa Misaada ya kuonekana wakati ndugu zao wanakufa kwa njaa.