Breaking: Haji Manara Aachiwa kwa Dhamana

Msemaji wa Simba, Haji Manara ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi Tanzania kwa takribani wiki moja.

Manara alishikiliwa akihojiwa siku moja tu baada ya kutekwa kwa mwanachama maarufu wa Simba, Mohamed Dewji.

Dewji maarufu kama Mo, alitekwa na watu wasiojulikana wakielezwa ni raia wa kigeni akiwa anaingia gym, alfajiri ya Alhamisi iliyopita.

Baada ya hapo, Jeshi la Polisi lilianza uchunguzi wa kina na Manara alikuwa kati ya watu waliochukuliwa kuhojiwa.